Kitabu cha Mbinguni

Wito wa Kiumbe kwa Utaratibu, Mahali na Kusudi ambalo Kwa ajili yake Aliumbwa na Mungu.

Siku Mpya Inaponza, Katika Utashi Wako, Ninakusifu Na Ninakupenda Ewe Baba Yangu!

** Ee Bwana ufungue midomo yangu
** Na Utashi Wako usali na kusifu ndani yangu


Ewe Baba na Muumba Wangu, Mimi nanajiyeyushia ndani ya bahari kuu ya Utashi Wako Mkuu wa juu. Pindi macho yangu yanapofunguka na kuona mwanga wa siku mpya, natamani nafsi yangu yote iamke toka pande zote za bahari kuu ya Mwanga wa Utashi Wako. Ni ndani ya Utashi huu peke yake ninapenda niwe ninaishi, ninafikiri,  inapumua, na niwe ninapenda. Ni ndani ya mipaka yake, mimi ninataka niwe ninazunguka daima ili kuandamana nao katika kila kazi yake. Ndani yake, Ewe Baba, napenda niwe ninakutolea ‘Ninakupenda’ yangu!’ 

Ni kweli, Baba Mtakatifu, ninataka tendo langu la kwanza kabisa la siku hii ya leo na liwe ni tendo la pendo kwako katika Utashi Wako wa Kimungu. Na katika Utashi Wako nitazunguka popote kutembeza Ninakupenda yangu ya kwanza katika kila silika ya uelewa iliyoumbwa, katika kila silika ya mtazamo wa kibinadamu, katika kila neno, katika kila kazi, hatua, katika kila pigo la moyo na pumzi ya mwanadamu.

Katika lile tendo moja pekee na la milele la Utashi Wako wa kimungu, ningependa kuja pamoja Nawe hadi kufika pale bustanini Eden, ili nikafungilie tendo langu la Pendo, na pendo la wanadamu wote, kwenye matendo yale  aliyokuwa yamefanywa na Adamu katika Utashi Wako Mtakatifu, na kwenye matendo yale yote watakayotenda  anadamu watakaokuja kuishi katika Utashi wa Mungu. Kwenye 5matendo hayo yote, nitafungilia hadi lile tendo la  wisho kabisa, ambalo watakuja kulitenda ndani ya Utashi huo hapa duniani.

Ninapoambatana Nawe hadi kule kwenye mipaka isiyokoma ya Utashi Wako, mimi nitajiinua kidogo juu pale katika  umbwa. Wewe umeumba kila kitu kwa ajili ya kumpenda binadamu na kwa ajili ya kunipenda mimi. Kwa ajili yangu  imi Wewe umesambaza Pendo Lako ndani ya kila kitu: Umelisambaza Pendo Lako ndani ya jua, ndani ya nyota,  dani ya bahari, umesambaza juu ya ardhi, ndani ya ndege, na ndani ya ua. Kwa ajili yangu, umeingiza Ninakupenda Yako ndani ya kila kitu.

Tazama sasa, Ewe Baba na Muumba Wangu, Pendo hilo lote  lilolisambaza kwa ajili yangu, mimi ninalitwaa, ninalifanya liwe ni la kwangu, na ninalitolea Kwako Mwenyewe kama  atendo mbalimbali ya heshima, ya upendo, ya kutukuza, ya sifa na shukrani mbalimbali, na ya utukufu Kwako Wewe. Na ninapoendelea kuzunguka ndani ya Utashi Wako, ninazidi kupanda juu zaidi, juu kule Paradisini, ili kuwatembelea Malaika na Watakatifu wote. Ninajiunga na hilo jeshi lote la Mbinguni, ili kwa niaba ya watu wote,  a kwa niaba ya kila mmoja wao, niweze kukupatia tendo langu la upendo, Ninakupenda yangu kwa ajili Yako Wewe  we Yesu uliye Chema Changu Kikuu na cha juu.

Halafu, ninapojongea kwa Malkia wa Mbinguni, aliye Mama Yako na Mama yangu Mtamu, toka kwake ninamwomba anipe matendo yake na mastahili yake yote. Yeye ananikabidhi kila kitu. Na mimi, katika imani ya mwanae mdogodogo, ninatwaa hayo yote, yaani, kila kitu alichokuwa amekitenda tangia kutungwa kwake  kiimakulata katika mimba, hadi siku ile ya pumzi yake ya mwisho. Na kana kwamba kila kitu kingekuwa sasa ni cha kwangu, mimi ninatolea kila kitu Kwako Wewe, uliye ni Ukuu Mtukufu wa juu kabisa. Natolea kila kitu Kwako, kama tendo langu la heshima iliyo nzuri kabisa kabisa kupita zote.

Na ninakujia Wewe, Ee Neno la Mungu uliyejifanya mtu, ili nikuombe unifanye niwe mshiriki wa matendo Yako yote: niwe mshiriki wa Kutungwa Kwako katika mimba, wa Kuzaliwa Kwako, wa tendo la kukimbilia Kwako Misri, niwe mshiriki wa ile miaka Yako thelathini ya maisha Yako ya kificho, na niwe mshiriki wa ile miaka Yako mitatu ya maisha ya utume Wako hadharani. Nataka niwe mshiriki wa Mateso Yako, niwe mshiriki wa kila tone la Damu Yako, mshiriki wa Kifo Chako na wa Ufufuko Wako na wa Kupaa Kwako mbinguni. Wewe ulikuwa umetekeleza hayo yote kwa ajili ya wanadamu wako na kwa ajili yangu mimi, na unayatoa yote kwangu mimi. Nami ninatwaa yote na kuyafanya yawe ya kwangu. Kishapo ninayatolea yote kwa Utatu Mtukufu, kwa heshima ya utukufu na kwa heshima ya pendo la shukrani.

Kwa minajili hiyo, ingawa kama mimi ni mwanadamu niliye duni kabisa, sasa ninaweza kukutolea Wewe tendo
langu la upendo. Ni kwa mtindo huo tu, Pendo hilo limeweza kuwa ni tendo timilifu na takatifu kabisa, kwani mimi
sikupatii chochote kilicho cha kwangu, bali, ninakurudishia Wewe, Ee Baba Yangu, ninakurudishia ule utukufu wote,
unaokujia kutokana na kile ambacho Wewe Mwenyewe umekwisha kukitenda, yaani, ule utukufu ambao ndio peke
yake unastahilika Kwako Wewe uliye ni Mungu. Basi, Ewe Baba Yangu, mimi ninakupenda katika Utashi Wako!

Katika Utashi Wako ninapenda nikuitikie kwa ajili ya Pendo lote ulilolisambaza kwa ajili yangu katika kazi Yako ya
Uumbwa, katika kazi Yako ya Ukombozi na katika kazi yako ya Utakaso.

Katika Utashi Wako ninataka nikupatie utukufu ule wote wa Kimungu ambao ni haki na stahili Yako, na ambao Wewe unautegemea toka kwa kila binadamu Wako. 

Kwa niaba yangu mwenyewe, na kwa niaba ya kila mwanadamu wako, ninakuja kwako katika Utashi Wako, ili kusudi nikusanye ule uhai mbalimbali wote wa Kimungu ambao Pendo Lako limeuandaa kwa ajili yangu mimi na kwa ajili ya ndugu zangu wote, na ambao sisi, katika utovu wetu wa shukrani, hatukutaka kuupokea. Ndiyo maana mimi ninakuja, Ewe Baba, ili, katika upendo, niweze kukulipa kwa kila aina ya uhai Wako.

Little Chaplet of the Divine Will

Saint Hannibal di Francia was one of Luisa’s extraordinary Confessors. So inspired was he by the spirituality of Luisa’s writings that he founded two Religious Orders: the Rogationist Fathers and the Daughters of the Divine Zeal. He was beatified by Pope John Paul II on 7 October 1990, and canonized on 16 May 2004. In the later years of his life he composed the following simple chaplet to be said on Rosary Beads. Every day he prayed this chaplet, often more than once, especially in his last sickness.

1

Begin

1 x Our Father, 1 x Hail Mary, 1 x Glory Be
2

On the Large Beads

Glory be ...
3

On the Small Beads

Thy will be done on earth, as it is in Heaven.
4

In conclusion

Lord Jesus,
we praise You, we love You, we bless You and we thank You together with the Father and the Holy Spirit in Your Holy and Eternal Divine Will.
Amen.

Maombi ya Kutangazwa kwa Luisa

Ee Moyo Mtukufu wa Yesu Wangu, Wewe, katika mtumishi wako mnyenyekevu LUISA umechagua tarishi wa Ufalme wa Utashi Wako wa Kimungu, na umemfanya awe Malaika wa kulipa fidia kwa makosa mengi yasiyo na idadi yanayotia uchungu na mateso katika Moyo Wako wa Kimungu, mimi, kwa unyenyekevu wote ninakuomba unijalie neema ambayo, kwa maombezi yake, ninakusihi katika Huruma Yako, ili atukuzwe hapa duniani kama vile ulivyokwisha kumtuza huko Mbinguni.

Amina.

Baba Yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba Ewe Moyo wa Kimungu wa Yesu Wangu, huyu Mtumishi Wako mnyenyekevu Luisa, mhanga wa Pendo Lako, katika muda wote wa maisha yake marefu, Wewe ulimpatia nguvu ya kuvumilia maumivu makali ya Mateso yako ya uchungu.

Fanyiza kwamba, kwa ajili ya utukufu Wako mkuu, lile taji la dhahabu la Wenye Heri, ling’ae upesi juu ya kichwa chake. Na kwa maombezi yake unijalie mimi neema hii niombayo kwa unyenyekevu.

Baba Yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba.Ewe Moyo wa Huruma wa Yesu Wangu, Wewe, kwa ajili ya wokovu na utakaso wa roho nyingi kabisa, umependa, kwa miaka mingi sana, kumhifadhi hapa duniani mtumishi Wako mnyenyekevu LUISA, Binti Yako Mdogo wa Utashi wa Mungu, naomba uisikilize sala yangu: kwamba, yeye huyo atukuzwe upesi kabisa na Kanisa Lako Takatifu. Na kwa maombezi yake unijalie mimi neema nikuombayo kwa unyenyekevu........

Baba Yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba.

Ee Bwana Wangu Yesu Kristo, Wewe unayetamani sana kwamba Utashi Wako wa Kimungu usimike Ufalme Wake 
hapa duniani kama vile kule mbinguni, ninakuomba sana, upende kumtukuza mtumishi Wako LUISA, Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu. Yeye alikwisha kukutukuza sana hapa duniani kwa fadhila zake za pekee kabisa, ulimpamba kwa juhudi zake motomoto, ukampamba kwa maandishi yake, na kwa maisha yake yote kwa ajili ya wokovu na utakaso wa roho mbalimbali zilizokombolewa kwa Damu Yako Azizi.

Amina.

Udruga Fiat Voluntas Tua, OIB: 29109364221, Giardini 4, 52100 Pula, Croatia

E-mail: admin@fiatvoluntastua.info
Statut udruge